Mfanyakazi katika chama cha
Republican nchini Marekani amejiuzulu baada ya kukosolewa kwa kuwatuhumu wanawe
Rais wa Marekani Barack Obama , Sasha na Malia kwa kuwaambia kuwa wamekosa
ustaarabu.
Elizabeth Lauten, afisaa mkuu wa
mawasiliano wa mwanasiasa mkuu wa chama hicho, Stephen Fincher, alijiuzulu
Jumatatu.
Bi Lauten, aliwakosoa watoto wa
Obama Sasha na Malia kwenye ukurasa wake wa Facebook baada ya watoto hao
kuonekana wakiwa wamevalia sketi fupi kwenye hafla ya jioni.
Baadaye Lauten alifuta maandiko
yake ambayo baadaye aliyataja ya kuumiza moyo na kuudhi.
Bi Lauten pia alikuwa amewakosoa
Sasha na Malia kwa kusema walionekana wasio na furaha walipokuwa wamesimama na
baba yao katika hafla ya maankuli katika Ikulu ya White House.
Wakati watu wengi walihisi kwamba
Sasha na Malia hawakua na furaha kuwa na baba yao katika hafla ile na hata
kulizungumzia swala hilo kwenye mitandao ya kijamii,Bi Lauten aliamua kujitoa
kimasomaso na kuwakosoa wasichana hao kupitia kwa Facebook.
Mwanamke huyo akiomba msamaha,
alisema baada ya kufanya maombi na hata kuzungumza na wazazi wake na kisha
kusoma maandiko yake kuwahusu Sasha na Malia, alihisi kweli aliwakera wasichana
hao.
"ningependa kuomba radhi kwa
wote niliowaudhi kwa matamshi yangu, na nina ahidi kujifunza na kubadilisha
mwenendo wangu, '' alisema Lauten".
Post a Comment